About Me

My photo
My Name is Neema Ng'asha C.E.O and Founder member of Strong Women Foundation.(SWF).

Saturday, October 9, 2021

NEEMA NG'ASHA ATOA VIDEO MPYA ASANTE.

 Muimbaji wa nyimbo za injili Neema Ng'asha jana ametoa video yake mpya inayoitwa "ASANTE". Neema Ng'asha amekuwa kimya kwa muda mrefu hajatoa video mpya lakini mwaka huu anamshuru Mungu kumuwezesha kufanya video hii.


Wimbo wa ASANTE ni wimbo wa shukrani unaolelezea wema wa Mungu maishani kwetu.

Kazi hii nzuri imefanywa na Director IPMAGERA kutoka jijini,Mwanza.

Audio imefanywa na producer Justin Rider kutoka Mwanza pia.

Nakusogezea kazi hii naamini itakuvusha kutoka kiwango kimoja cha imani kwenda kiwango kingine.

Fanya kubonyeza link kuangalia wimbo wote

👇👇👇👇👇👇👇🔥🔥💦💧💥

https://youtu.be/BISujOEKqZU


Saturday, June 6, 2020

NEEMA NG'ASHA ATOA WIMBO MPYA THANK YOU.

Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini,Mwanza ametoa wimbo mpya THANK YOU.

Bonyeza link hii kusikiliza.
https://youtu.be/1bS7pKjBkq0




Friday, January 31, 2020

NEEMA NG'ASHA AACHIA WIMBO MPYA UMEINULIWA.

Habari Njema kutoka jijini Mwanza kwa mara ya kwanza katika mwaka 2020 tumekusogezea wimbo mpya wa kuabudu unaoitwa UMEINULIWA kutoka kwa Neema Ng’asha.
Karibu kusikiliza wimbo huu mzuri na hakika utabarikiwa na kuinuliwa, Eimen.

Tuesday, August 27, 2019

NEEMA NG'ASHA ATOA WIMBO MPYA "WEWE NI MUNGU"


Kutoka Tanzania kwa mara nyingine tena tumekusogezea wimbo mpya wa kuabudu kutoka kwa Neema Ng’asha mwimbaji wa nyimbo za Injili akitokea jijini Mwanza.
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza wimbo huu mzuri ambao kwa hakika utakubariki, Amen.

Kusikiliza wimbo huu bonyeza link hii.

 https://youtu.be/Ind1JJedNMk

Saturday, August 3, 2019

NEEMA NG'ASHA KUFANYA LIVE CONCERT (IN HIS PRESENCE SEASON ONE )

Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jiji Mwanza,Neema Ng'asha anatarajia kufanya tamasha la kusifu na kuabudu(IN HIS PRESENCE LIVE CONCERT SEASON ONE) ambapo siku hiyo atazindua album ya "AKISEMA NDIYO".Tamasha hilo litafanyika tarehe/2019 Katika kanisa la MICC,Nyegezi kwa Dr.Zakayo Nzogere.Neema Ng'asha amewakaribisha Wadau wote wa muziki wa injili kuja kwa wingi kumuabudu Mungu kwa pamoja.Waimbaji wengi wamethibitisha kuwepo siku hiyo kumtia moyo Neema Ng'asha.

Thursday, January 24, 2019

NEEMA NG'ASHA KUACHIA WIMBO MPYA" NI WAKO"


Kwa mara nyingine tena muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza,Neema Ng'asha anatarajia kuachia kazi yake mpya iliyo katika mfumo wa audio inayoitwa"NI WAKO"
Neema Ng'asha ambaye kwa sasa nafanya kazi chini ya usimamizi wa NZALI NEXT LEVEL PROMOTION amesema kazi hiyo itakuwa tayari hivi karibuni kwa hiyo anaomba wadau wote wa nyimbo za injili wafatilie katika youtube account yake"Neema Ng'asha na Youtube account ya Nzali Next Level pia katika ukurasa wa facekoob wa Neema Ng'asha na Nzali Leonard.
Wimbo wa"NI WAKO" Umefanywa na Producer Ben William kutoka studio za APEX MUSIC, Mwanza.

NEEMA NG'ASHA ALAMBA DILI NZALI NEXT LEVEL PROMOTION.

Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini,Mwanza Neema Ng'asha ameingia mkataba wa kusimamiwa kazi zake za uimbaji na kampuni ya NZALI NEXT LEVEL PROMOTION iliyoko nchini Marekani. Akiongea na mwandishi wetu Neema Ng'asha anasema anamshukuru sana MUNGU kwa hatua hii aliyofikia sababu lilikuwa ni ombi lake la muda mrefu sana. Neema Ng'asha anasema "NIMEJIFUNZA KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA" anazidi kusema amepitia changamoto nyingi sana ambazo bila msaada wa Mungu asingeweza kuendelea na huduma.Lakini leo anasema amemuona MUNGU akifanya njia pasipo na njia.
Neema Ng'asha anapenda kuwatia moyo waimbaji wengine wanaonza huduma wasikatishwe tamaa na mazingira magumu wanayopitia"WAMTEGEMEE MUNGU KWA MAJIRA NA WAKATI WAKE HUFANYA KILA KITU KWA UZURI"
Neema anapenda kumshukuru meneja wake Leonard Nzali  ambaye makazi yake kwa sasa ni nchini Marekani, kwa kumpa nafasi hii kufanya nae kazi ili kulitangaza neno la Mungu liwafikie watu wengi.